SIRI KUU3 ZA KULINDA SIRI ZAKO ZOTE
Prophet Samson Oxpel Mboya
Utangulizi:
Kila aliyefanikiwa hapa Duniani ana siri ya mafanikio yake, Na adui yeyote anayepambana au anayetaka kupambana Na wewe anaitafuta siri yako, sasa Ili ufanikiwe katika jambo lolote katika maisha yako lazima uwe Na siri jifunze siri ya kutunza siri zako, katika maisha yako lazima uwe na siri,
Siri ni nini?
Siri ni mipango iliyo ndani ya moyo wa mtu juu ya hatima ya maisha yake,
Mithali 16:1 Maandalio ya moyo Ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka Kwa Bwana kila jambo unalolipanga ndani ya Moyo wako fahamu hiyo ndiyo siri yako, hakuna mtu awezaye kufahamu mipango iliyo ndani ya mtu bila kuambiwa, watu wengi wamevuruga maisha yao bila ya kujuwa sababu ni ipi,
Kuna watu wamefukuzwa kazi na wengine wameshushwa veo kwa sababu ya kutoa siri zao wengine wameharibu biashara wengine masomo wengine uchumba wengine ndoa zao zimevunjika kabisa, kwasababu ya kutoa siri Sasa Mungu ametupatia nafasi hii tujifunze ili tupate maarifa ya kutunza siri zetu
Mithali 1:7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Kumchabwana bwana ni kumtumaini Mungu kwa kila jambo lako na kuyashika maagizo yake yote na kuyatenda ndipo atakupatia maarifa na hekima ya hatima ya maisha yako, ila utapodharau mafundisho ya Mungu hayatakusaidia popotekwa kalolote,
Kwakuwa maandiko yametufundisha kuwa siri hukaa moyoni mwa mwanadamu basi shughuli kubwa kumbe inafanyikia moyoni mwa i, hivyo kumbe ili ufanikiwe unatakiwa kujuwa siri ya siri ya kutunza siri zilizo moyoni mwako,
v Hatua ya kwaza ya kulinda siri zako,
Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Siri ya kwaza ya kulinda siri zako ni kuulinda Moyo wako maana ndiko mipango yote inafanyikia na ndiyo sehemu salama ambayo hakuna mtu awezaye kujuwa unapanga nini juu ya maisha yako, ninafahamu kila mtu ana mipango mingi au kidogo juu ya hatima ya maisha yake ila Mipango mingi haijakamilika sababu ya kutoa siri ya mipango yako kabla hata haijakamilika,
Siri ya 1ya kuilinda siri zako soma mithali 4;23- Ni kulinda Moyo wako,
v Siri yako ndiyo mafanikio yako yote
v Siri yako ndiyo mipango yako yote
v Siri yako ndiyo Maisha yako yote
v Siri yako ndiyo uzima wako wote
Kufanikiwa au kuinuliwa na Mungu kunatokana na wewe kutotoa siri yako kwa Mtu yeyote Yule, awe Rafiki au mchumba, mke,Mme,Baba au Mama usikubali kutoa siri zako au kuwaambia ambia watu mipango ya moyoni Mwako,
Yapo madhara unayoweza kuyapata kama utatoa siri yako kwakuwa watu wengi wanataka kujuwa siri yako wakiijuwa haya mambo yanaweza kukutokea maishani mwako
v Kushikwa kazi au biashara,uchumba,ndoa,mausiano
v Kufungwa kazi au biashara,uchumba,ndoa,mausiano
v Kuteswa katika kazi au biashara,uchumba,ndoa,mausiano
v Kushindwa katika kazi au biashara,uchumba,ndoa,mausiano
Hapa kuna mtu anayejifanya anajuwa kupenda akatoa siri yake angalia kilichompata,Huyu Dada bado alikuwa Mchumba lakini anaanika siri zote,
Waamuzi 16:4- ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke katika
mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila.
Nao wakuu Wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua (siri ) ya sili ya nguvu zake nyingi, Na jinsi tutakavyoweza (kumkamata) kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
Nao wakuu Wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua (siri ) ya sili ya nguvu zake nyingi, Na jinsi tutakavyoweza (kumkamata) kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
Kwa hasara iliyokuwa imesababishwa na Samson hapa walichokitaka ikiwezekana ni kumuuwa Samsoni ila wafanyeje ndiyo ilikuwa kazi kwao maana walikuwa hawajui siri ya samsoni, Sasa watu wameamua wamtafute mtu wakaribu na wakamshawishi kwa hela nyingi kama unavyojuwa hela ni kishawishi kikubwa sana kwa mwanadamu, pamoja na Yuda kuwa mwanafunzi wa Yesu kristo anayependwa bado alitoa siri ili Yesu apatikane
Usipende kutoa siri zako kuna watu wako tayari kutoa fedha nyingi kwa watu wako wa karibu ili waijui siri yako,ili wakuangamize kabisa,
Ukisikia benk wameibiwa kuna mtu ametoa siri ukisikia jeshi limevamiwa kuna mtu akatoa siri kuona ndoa,uchumba imevunjika kuna mmoja ametoa siri kila jambo linalotokea katika maisha yako jua ukifanikiwa siri bado haijavuja na ukiona mambo yanaanza kuharibika jua siri imeanza kuvuja,
siri yako ndiyo Maisha yako na uhai wako,
Waamuzi 4:17-22`Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikilia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.
Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti.
Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti.
Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika.
Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu awaye yote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana.
Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu awaye yote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana.
Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.
Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonyesha yule mtu unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake.
Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonyesha yule mtu unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake.
Huyu amepokelewa na akaambiwa usiogope akaomba maji akapewa maziwa la kini yote ya yote akauwawa, si kila anayekupa zawadi au kitu anakupa kwa uzuri inawezekana ni mtego ili ujisahau akukamati akufunge akutese mpaka kufa, usikubali kutoa siri yako hata iweje, kataa kabisa,usikubali kubembelezwe kwa maneno ya kusifiwa au kupewa zawadi au pesa, usitoe siri yako,unaweza ukayapoteza maisha yako kama mchezo tu,
Siri ya 2 ya kulinda siri zako
Kwakuwa siri zote ndiyo mipango yetu yote ya moyoni unatakiwa kuwa makini na kujiadhari sana na wale watu wote wa karibu yako, kwa mfano wazazi,mke au mme,mchumba,mfanyakazi mwezako,mfanyabiashara mwezako,Rafiki yako wa karibu usiwaamini kupita kiasi na kuanza kuwaambia siri zako zote, inawezekana Hapo ulipo unaulizana swali saa hii sasa ya kwamba Nabiiu uanasema nini soma Mathayo 10:36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake
Haya siyo maneno yangu na Maneno matakatifu yaliyotoka katika bibilia takatifu, Mimi niko hapa kukusaidia wewe ujuwe milango adui anayoweza kupitia ili akukamateme
Ukisoma sehemu nyingine maandiko yanaongelea juu ya Mungu kuwa na Siri,
Kumbukumbu la torati 29:29 Mambo ya siri Ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa Ni yetu sisi Na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.
Kumbe kuna mambo ambayohatuyajui hatujayajuwa na hatutayajuwa kutoka kwa Mungu Hadi ametaka tuyajuwe Zaburi 25:14 Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake. Kwahiyo kumbe hata kuyajuwa mambo ya Mungu ni lazima uwe mchaji wake ili aweze kukupatia siri ambazo hajaambia wengine,
Somo hili limebeba siri kubwa sana zipo sehemu nyingi sana katika maandiko matakatifu yanayoongelea kuwa hata Mungu ana siri hiyo ndiyo sababu kuu ya somo hili
Marko 13:31-32 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Kuna matukio Malaika wa Mbinguni au Mwana haji Hiyo ni siri Ya Mungu sasa kama Mungu anayosiri wewe Pepepepe ni za nini? Ficha siri yako mwache Mungu achunguzae miyoyo ajuwe si mwanadamu,kama wewe,
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Kuna matukio Malaika wa Mbinguni au Mwana haji Hiyo ni siri Ya Mungu sasa kama Mungu anayosiri wewe Pepepepe ni za nini? Ficha siri yako mwache Mungu achunguzae miyoyo ajuwe si mwanadamu,kama wewe,
Usikubali kusema siri zako kwa Mwanadamu yeyote Yule Hata kama ni kiongozi wako mahali pa kazi au biashara au Rafiki mlioshibana kushibana ni maneno tu hayo huyo huyo unayesema mmeshibana ndiye adui yako mkubwa
Mika 7:5-6 Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari
Sir ya 3 kutomwamini mwanadamu yeyote Yule wala kumuwekea tumaini na kutokubali kufunguwa Mlango wako ovyo ovyo yaani kinywa chako kiwe na ukiasi na kichaguwe maneno ya kuongea na yakutoongea, ukilinda mdomo wako vizuri kwakutu toa siri zako kutomchokoza Mungu kwa kinywa chako Moyoni mwako kutakuwa salama na siri zako zitakuwa salama zote na hatima ya maisha yako itakuwa tofauti sana na wengine utajishangaa wewe na wengine watakushangaa pia, sasa weka kitanzi kinywani mwako kwanzia sasa juu ya siri zako
Muhubiri 5:6 Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?
Kinywa chako kinauwezo wa kuusababishia Mwili wako matatizo usipikuwa makini nao, pia kila mwanadamu Mungu amempa malaika wa kuwa naye wakati wote anapotenda matendo mema ya Mungu ukimkosea huyu malaika umemkosea Mungu mwenyewe, na Mungu ataharibu kazi ya mikono yako chunga sana kinywa chako
Inawezekana umenuniana na jirani yako kwasababu ya kinywa chako au umenuniana na mkeo au mmeo motto kwa sababu ya kinywa juwa kwamba humkomoi mtu bali unamkasirisha Malaika wa Mungu na Mungu akikasirika imekula kwako mali zako zitapukutika kama maua
Kama unaona huelewani na watu kwasababu yakinywa chako tafuta watumishi wa Mungu wakushahuri na kukuombea ili uwe salama vinginevyo ni hatari sana kutumia kinywa vibaya
Ushahuri wangu wa bure kabisa kama Nabii wa Bwana nakuomba ili siri zako zisitoke punguza maneno kinywani mwako kama siyo kunyamaza kabisa kwa mambo yasitakiwa kusema, Mathayo 5:37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu
Kwa ajili ya kupata CD/DVD/VCD YA SOMO Hili wasliana na Prophet Samson
0756 809 209